Maudhui ya Vurugu na Michoro

Maelezo ya sera

BADILISHA KUMBUKUMBU
Utaratibu wa Sera
Tunaelewa kuwa watu wana hisia tofauti kuhusiana na maudhui ya michoro na vurugu. Ili kuwalinda watumiaji dhidi ya maudhui kama hayo, tunaondoa maudhui ya michoro zaidi na kuongeza lebo za tahadhari kwa aina nyingine ya maudhui ili watu wawe wanafahamu kwamba yanaweza kuwa nyeti kabla ya wao kuyabofya. Tunazuia uwezo wa vijana kuona maudhui ambayo huenda hayawafai kulingana na umri. Kwa kufanya hivyo, tunalenga kutoa hali ya matumizi ya mtumiaji inayofaa, huku tukiendelea kutoa nafasi kwa watumiaji wetu kujieleza.
Tunatambua kwamba watumiaji wanaweza kushiriki maudhui ili kufafanua au kushutumu matendo kama vile matumizi mabaya ya haki za binadamu au vurugu ya kutumia silaha. Sera zetu zinazingatia wakati ambapo maudhui yalishirikiwa katika muktadha huu na kutoa nafasi ya majadiliano na uhamasisho ipasavyo.
Katika matangazo ya kulipiwa, tunatoa ulinzi wa ziada. Kwa mfano, maudhui ambayo yamechukuliwa kuwa nyeti hayajatimiza masharti ya kuendeshwa katika matangazo. Pia tunapiga marufuku matangazo kujumuisha picha na video ambazo zinatisha, za kuogofya au vinginevyo ni za ajabu. Kupata maelezo zaidi, tafadhali rejea Viwango vyetu vya Utangazaji.
Usichapishe:
Taswira za watu
Video za watu, walio hai au waliofariki, katika miktadha isiyo ya kimatibabu, inayoonyesha:
  • Kukatwa viungo.
  • Viungo dhahiri vya ndani, kama vile viungo, mifupa au misuli iliyo kwenye watu walio hai au waliofariki.
  • Watu wanaochomeka; au
  • Kukatwa koo.
Kutitirisha moja kwa moja adhabu kuu.
Maoni ya Kikatili
Maoni ya kikatili ni maoni – kama vile manukuu au maoni – yanayoonyesha furaha au kuridhika kutokana na maumivu au kudhalilishwa kwa watu au wanyama.
Tunaondoa
  • Maoni ya kikatili yanayotolewa kuhusu picha (iwe ni video au picha tuli) ambayo vinginevyo hupewa skrini ya onyo chini ya sera hii, inayowaonya watu kuwa huenda maudhui hayo yakawa nyeti; isipokuwa ikiwa picha hizo zinaonyesha vitendo vya kujikinga (k.m., video ya mtu anayejitetea dhidi ya wizi wa mabavu) au aliye katika muktadha wa kimatibabu (k.m., picha ya wataalamu wa matibabu wanaofanya zoezi la upasuaji).
  • Maoni ya moja kwa moja ya kikatili yanayofanywa kuhusu kuumia kwa wanyama wanaoonyeshwa kwenye picha, na picha inayoonyesha wanyama waliokuwa hai wakifa.
  • Kupeana au kuombaomba taswira ambayo imefutwa au iliyowekewa skrini ya onyo chini ya sera hii, kwa kuambatana na maoni ya kikatili.
Kwa maudhui yafuatayo, tunajumuisha skrini ya onyo ili watu wafahamu kuwa huenda maudhui yakawa nyeti. Pia tunaweka mipaka ya uwezo wa kutazama maudhui kwa watu wazima, wa umri wa miaka 18 na zaidi:
Taswira za watu
Video za watu, walio hai au waliofariki, katika miktadha ya kimatibabu, inayoonyesha:
  • Kukatwa viungo.
  • Viungo dhahiri vya ndani, kama vile viungo, mifupa au misuli iliyo kwenye watu walio hai au waliofariki;
  • Watu wanaochomeka, ikiwa ni pamoja na miktadha ya uchomaji wa miili ya wafu; au
  • Kukatwa koo.
Picha tuli za watu, walio hai au waliofariki, zinazoonyesha:
  • Kukatwa viungo.
  • Viungo dhahiri vya ndani, kama vile viungo, mifupa au misuli iliyo kwenye watu walio hai au waliofariki.
  • Watu wanaochomeka; au
  • Kukatwa koo.
Taswira (video pamoja na picha tuli) inayoonyesha kifo cha vurugu cha mtu (ikiwemo wakati wa kifo chake au baada) au mtu aliyekabiliwa na tukio la kutishia maisha (kama vile kugongwa na gari, kuanguka kutoka kimo kirefu, au kupata jeraha lingine linaloweza kusababisha kifo).
Taswira inayoonyesha adhabu kuu kwa mtu (bila kujumuisha mitiririko ya moja kwa moja).
Picha inayoonyesha vitendo vya ukatili (k.m., vitendo vya vurugu au matishio mabaya dhidi ya wahusika waliozuiliwa kwa nguvu) dhidi ya watu au kikundi cha watu.
Taswira zinazoonyesha vifaa vya nje vya matibabu na visivyo vya matibabu (kwa mfano., visu, misumali au vifaa vingine vya chuma) vilivyochoma ngozi ya mtu;
Taswira zinazoonyesha meno ya mtu yaliyovunjika, kutokwa damu au kung’ooka ambapo kuna damu; au kuwekwa kwa vitu vya nje kwenye meno au fizi.
Taswira zinazoonyesha vijusi na watoto walio nje ya tumbo la uzazi ambao wamekufa, isipokuwa kama kuna mtu mwingine kwenye picha.
Taswira za wanyama
Taswira zozote za wanyama, walio hai au kufa, – zinazoonyesha kukatwa viungo, viungo vya ndani vinavyoonekana, kuchomeka au kuchemshwa wakiwa hai.
Taswira za wanyama waliokuwa hai, wakifa.
Taswira za binadamu wanaotenda vitendo vya ukatili dhidi ya wanyama walio hai (k.m, kupiga teke, kuzama majini au kubambua manyoya).
Kwa maudhui yafuatayo, tunaweka kizuizi cha uwezo wa kuyatazama kwa watumiaji wenye umri wa miaka 18 na zaidi:
Taswira za watu
Picha zinazoonyesha miili za watu waliokufa ambayo imefunikwa kiasi au haijafunikwa kabisa, hata kama hakuna viashiria vya kifo cha vurugu.
Taswira zinazoonyesha vijusi na watoto walio nje ya tumbo la uzazi ambao wamekufa, wakati kuna mtu mwingine kwenye picha.
Picha zinazoonyesha sindano zinazochoma ngozi ya mtu katika muktadha usio wa kupata chanjo, tiba vitobo, kuchora chale au kujitoboa.
Taswira zinazoonyesha watu waliojeruhiwa katika miktadha ya matibabu wanapoonekana kupitia maumivu au mfadhaiko, kuumia au kwa tubu za kimatibabu kwenye nyuso na/au mikono yao.
Picha zinazoonyesha uchafu au ugiligili wa mwili (kwa mfano, mavi, mkojo, tapiko, nta ya sikioni, makamasi, bidhaa zinazotolewa kwenye ngozi au damu).
Picha zinazoonyesha magari yanayochomeka au kulipuka, au kuonyesha tukio au baada ya gari linalooendeshwa kwa kasi kugongana na vitu vingine ambapo gari limeondolewa kwenye njia yake na / au sehemu ya dereva au abiria zimeharibika vibaya sana.
Taswira za wanyama
Taswira zinazoonyesha wanyama, walio hai au kufa, ambapo kuna damu inayoonekana.
Picha zinazoonyesha wanyama katika muktadha wa kuzaa (m.f., kuna damu au viungo vya ndani vinavyoonekana).
Picha zinazoonyesha wanyama walio hai au kufa, ambapo wadudu wanaonekana kutoka kwa wanyama hao (k.m., funza).
Taswira zinazoonyesha wanyama waliojeruhiwa wakipitia mateso.
Taswira za Kubuni
Taswira zinazoonyesha watu wa kubuni katika miktadha ifuatayo:
  • Kukatwa viungo;
  • Viungo vya ndani vilivyo dhahiri, kama vile viungo, mifupa au misuli;
  • Watu wanaochomeka;
  • Kukatwa koo; au
  • Kifo cha vurugu au matukio ya kutishia maisha.
Taswira zinazoonyesha watu wa kubuni ambazo ni picha halisi (ambapo picha hizo zinafanana sana na picha au video ya mtu halisi) katika miktadha ifuatayo:
  • Vitu vya nje visivyo vya matibabu (kwa mfano., visu, kucha au vifaa vingine vya chuma) vilivyochoma ngozi;
  • Uchafu au ugiligili wa mwili (kwa mfano, mavi, mkojo, tapiko, nta ya sikioni, makamasi, au bidhaa zinazotolewa kwenye ngozi) bila kujumuisha damu;
  • Watoto au vijusi vilivyofariki vilivyo nje ya tumbo;
Picha inayoonyesha wanyama wa kubuni walio katika miktadha ifuatayo:
  • Kukatwa viungo;
  • Viungo vya ndani vilivyo dhahiri, kama vile viungo, mifupa au misuli;
  • Watu wanaochomeka au kugeuka nyeusi;
  • Wanyama wanaochemshwa wakiwa hai;
  • Damu ipo;
  • Wanyama waliokuwa hai, wakifa;
  • Watu wanaotenda vitendo vya ukatili (k.m, kupiga teke, kuzama majini au kubambua manyoya) kwa wanyama walio hai;
  • Wanyama waliojeruhiwa wanaopitia mateso
  • Wanyama wenye wadudu wanaotoka kwao (k.m., funza)
Kwa Viwango vya Jumuiya vifuatavyo, tunahitaji maelezo ya ziada na/au muktadha ili kutekeleza:
Haturuhusu:
Taswira au sauti za kifo cha vurugu cha mtu wakati kifo cha mtu kimethibitishwa kwenye rekodi za watekelezaji wa sheria, cheti cha kifo, ripoti ya Mshirika Anayeaminika au ripoti ya vyombo vya habari na mwanafamilia ya marehemu anaomba iondolewe.
Video ya binadamu wanaochomeka katika muktadha wa kujitoa kafara kama kitendo cha kuasi.
Tunaweza kuruhusu:
Taswira za kifo cha vurugu cha mtu au tukio linalotishia maisha wakati ni tukio linaloambatana.
Hali ya matumizi ya mtumiaji
Tazama mifano kadhaa ya jinsi utekelezaji unavyoonekana kwa watu kwenye Facebook, kama vile: inavyoonekana kuripoti kitu ambacho unafikiri hakipaswi kuwa kwenye Facebook, kuambiwa kuwa umekiuka Viwango vyetu vya Jumuiya na kuona skrini ya onyo juu ya maudhui fulani.
Dokezo: Tunaendelea kuboresha, kwa hivyo kile unachokiona hapa kinaweza kupitwa na wakati kiasi ikilinganishwa na kile tunachotumia sasa.
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Kuripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Mawasiliano ya baada ya ripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Hali ya kuondoa
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Skrini za onyo
Data
Tazama Ripoti ya sasa ya Utekelezwaji wa Viwango vya Jumuiya
Utekelezaji
Tuna sera sawa ulimwenguni kote, kwa ajili ya kila mtu kwenye Facebook.
Timu za ukaguzi
Timu yetu ya kimataifa ya wakaguzi zaidi ya 15,000 hufanya kazi kila siku kuweka watu kwenye Facebook kuwa salama.
Ushiriki wa mshikadau
Wataalamu wa nje, wasomi, mashirika yasiyo ya faida na watungaji sera husaidia kuweka Viwango vya Jumuiya ya Facebook.
Pata usaidizi wa maudhui ya vurugu na michoro
Jifunze unachoweza kufanya ukiona kitu kwenye Facebook ambacho kinakiuka Viwango vyetu vya Jumuiya.
Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi