Ukiukaji wa Faragha
Maelezo ya sera
BADILISHA KUMBUKUMBU
Leo
2 Okt 2024
26 Jun 2024
29 Jun 2023
23 Feb 2023
29 Sep 2022
24 Feb 2022
24 Nov 2021
30 Sep 2021
18 Nov 2020
30 Nov 2018
29 Jun 2018
Utaratibu wa Sera
Huduma zetu zinanuia kulinda faragha na taarifa binafsi za watumiaji wetu. Tunafanya kazi kwa bidii kulinda utambulisho wako wa kibinafsi na maelezo na hatuwaruhusu watu kuchapisha aina fulani za taarifa binafsi au za siri kuwahusu au kuwahusu wengine. Pia tunawapa watu njia za kuripoti taswira ambazo watu wanaamini kuwa zinakiuka haki zao za faragha.
Tunaondoa maudhui yanayoshiriki, kutoa, au kuomba taarifa inayomtambulisha mtu binafsi au taarifa nyingine ya faragha inayoweza kusababisha dhuluma ya kimwili au kifedha, ikijumuisha taarifa ya kifedha, makazi, na matibabu, sawa na taarifa ya faragha iliyotolewa katika vyanzo visivyo halali. Tunatambua kuwa maelezo ya faragha yanaweza kupatikana hadharani kupitia utangazaji wa habari, uandikishaji mahakamani, matangazo ya vyombo vya habari, au vyanzo vingine. Hiyo ikifanyika, tunaweza kuruhusu maelezo hayo yachapishwe.
Tuna vizuizi vya ziada katika maudhui yanayolipwa. Ingawa haturuhusu matangazo yanayotoa hali nzuri ya utumiaji kwa kulenga maelezo ya bidhaa au huduma, tunaondoa matangazo yanatumia vibaya hali ngumu za kibinafsi, yanayoonekana kutoa sifa mbaya au isiyo sahihi kuwahusu au kukisia kufahamu kuhusu taarifa nyeti ya kibinafsi. Kwa maelezo zaidi kuhusu kanuni za faragha za maudhui yanayolipiwa, angalia Viwango vyetu vya Utangazaji kuhusu Ukiukaji wa Faragha na Sifa za Kibinafsi.
Haturuhusu:
Maudhui yanayoshiriki au kuomba taarifa ya kibinafsi, kwenye huduma zetu au kupitia viungo vya nje: kama inayofuata:
Maelezo yoyote yanayoweza kumtabulisha (PII)
- Kushiriki Taarifa Inayomtambulisha Mtu (taarifa ambayo inamtambulisha mtu binafsi) ya bango au watu wengine. Haya ni pamoja na:
- Nambari za vitambulisho vya kitaifa kama vile nambari za ruzuku ya serikali (SSN), nambari za pasipoti au nambari ya utambulisho wa mlipa ushuru binafsi (ITIN)
- Vitambulisho vya serikali vya mtaalamu wa kutekeleza sheria, jeshi au mtaalamu wa usalama.
- Rekodi au waraka rasmi wa taarifa ya usajili wa kiraia kama vile hati za ndoa, kuzaliwa, kifo, kubadilisha jina au utambuzi wa jinsia
- Hati za uhamiaji na hali ya kazi kama vile kadi za kijani, vibali vya kazi au visa
- Maudhui yanayouliza Taarifa Inayomtambulisha Mtu ya wengine
Maelezo Yako ya Kibinafsi
- Maudhui yanayoshiriki maelezo ya kibinafsi ya mawasiliano ya watu wengine, isipokuwa zinapowekwa hadharani na mtu huyo binafsi au zinaposhirikiwa au kuombwa ili kutangaza sababu za hisani, kuwezesha kutafuta watu, wanyama, au wamiliki wa vitu vilivyopotea, au kuwasiliana na biashara au mtoa huduma (isipokuwa imethibitishwa kuwa maelezo ya kibinafsi ya mwasiliani yanashirikiwa bila ridhaa ya mtu binafsi).
Taarifa ya makao
- Kushiriki anwani kamili za makazi ya watu wengine, ikiwemo jina la jengo au alama kwenye ramani inayotambulisha anwani (hata kama alama ziko kwenye kiungo cha nje ya jukwaa), isipokuwa katika miktadha ifuatayo:
- inaposhirikiwa ili kukuza misaada, kuwezesha kutafuta watu waliopotea, wanyama au wamiliki wa vitu vilivyokosekana, au kuwasiliana na biashara au watoa huduma.
- wakati makazi hayo ni rasmi au yaliyotolewa na balozi kwa afisa wa kiwango cha juu kwa umma:
- Maudhui yanayoshiriki anwani za makazi za watu wengine (isipokuwa wakati makazi hayo ni rasmi au yaliyotolewa na balozi kwa afisa wa kiwango cha juu kwa umma):
- Zinaposhirikiwa katika muktadha wa kuandaa maandamano au ufuatiliaji wa mkazi na eneo la makazi hutambuliwa na mojawapo ya yafuatayo:
- Mtaa
- Jiji au ujirani (kwa miji iliyo na chini ya wakaazi 50,000 pekee)
- Msimbo wa posta
- Pin za GPS au pin kwenye ramani zinazotambua mojawapo ya hizi (hata kama pin ziko kwenye kiungo cha nje ya jukwaa)
- Picha inayoonyesha mwonekano wa nje wa makao ya kibinafsi iwapo hali zote zifuatazo zinatumika:
- Makao ni nyumba ya familia moja, au nambari ya kitengo cha makao/jina la jengo inatambuliwa katika picha/manukuzi.
- Eneo la makazi linatambuliwa na mojawapo ya yafuatayo:
- Mtaa
- Jiji au ujirani (kwa miji iliyo na chini ya wakaazi 50,000 pekee)
- Msimbo wa posta
- Pin za GPS au pin kwenye ramani zinazotambua mojawapo ya hizi (hata kama pin ziko kwenye kiungo cha nje ya jukwaa)
- Maudhui yanatambua makao.
- Aidha mkazi huyo anakataa makao yao ya kibinafsi kufichuliwa au kuna muktadha wa kupanga maandamano dhidi ya makao.
- Picha ya makazi haishirikishwi kwa sababu makao hayo ndiyo msingi wa habari (isipokuwa inaposhirikiwa katika muktadha wa kuandaa maandamano dhidi ya mkazi)
- Maudhui yanayoomba maelezo ya anwani za makazi za watu wengine (isipokuwa wakati makazi hayo ni rasmi au yaliyotolewa na balozi kwa afisa wa kiwango cha juu kwa umma)
- Maudhui yanayoomba eneo la nyumba salama auyanayoweka wazi taarifa kuhusu nyumba salama kwa kushirki yoyote kati ya yafuatayo, (isipokuwa wakati nyumba salama inatangaza taarifa kuhusu kituo chao)
- Anwani halisi (Kumbuka: "Sanduku la Posta pekee’ inaruhusiwa)
- Picha za nyumba salama
- Jiji/ujirani unaoweza kutambuliwa wa nyumba salama
- Taarifa inayoweka wazi utambulisho wa wakaaji wa nyumba salama
Taarifa ya matibabu
- Maudhui yanayoshiriki au kuomba maelezo ya wengine ya kimatibabu, kisaikolojia, kibayometriki au urithi wa maumbile (ikijumuisha yanapoonyeshwa hadharani au kushirikiwa kupitia sauti au video), wakati ni wazi kwamba maelezo hayo yanatoka kwa rekodi za matibabu au hati nyingine rasmi.
Taarifa ya kifedha
- Kushiriki maudhui au kuuliza maelezo ya kibinafsi ya kifedha kuhusu bango au wengine, yanayofafanuliwa kama maelezo kuhusu fedha za mtu binafsi ikiwemo:
- Rekodi za kifedha zisizo za umma.
- Nambari za akaunti ya benki zenye usalama au misimbo ya nenosiri.
- Taarifa ya njia ya malipo ya kidijitali yenye maelezo ya kuingia, usalama au misimbo ya nenosiri.
- Taarifa ya kadi ya mkopo au kadi ya malipo yenye tarehe za uhalali au misimbo ya usalama.
- Maudhui yanayoshiriki au kuuliza maelezo ya kifedha yasiyo ya umma ya biashara au shirika, yanayofafanuliwa kama maelezo kuhusu fedha za biashara au mashirika, isipokuwa yanaposhirikiwa na shirika lenyewe (ikiwemo ushirikishwaji unaofuata ulio na muktadha halisi) au kushirikiwa kupitia mahitaji ya kuripoti kwa umma (kwa mfano kama inavyotakikana na soko la hisa au mashirika ya udhibiti), ikijumuisha:
- Rekodi za kifedha zisizo za umma
- Nambari za akaunti ya benki Pamoja na misimbo ya usalama.
- Taarifa ya nia ya malipo ya kidijitali ikiwa Pamoja na maelezo ya kuingia, misimbo ya usalama.
Taarifa iliyotolewa kwenye vyanzo vilivyodukuliwa
- Maudhui yanayodaiwa na mchapishaji au yamethibitishwa kutoka kwenye chanzo kilichodukuliwa, licha ya iwapo mtu aliyeathirika ni mtu mashuhuri au mtu binafsi.
Pia maudhui yafuatayo yanaweza kuondolewa:
- Picha au video iliyoripotiwa ya watu ambapo mtu aliyeonyeshwa kwenye picha ni:
- Mtoto wa chini ya umri wa miaka 13, na maudhui yaliyoripotiwa na mtoto au mzazi au mlezi wa kisheria.
- Mtoto wa umri wa miaka kati ya 13 na 18, na maudhui yaliripotiwa na mtoto.
- Mtu mzima, ambapo maudhui yaliripotiwa na mtu mzima kutoka nje ya Marekani na sheria inayotekelezwa inaweza kutoa haki za uondoaji.
- Mtu yeyote mlemavu na hawezi kuripoti maudhui mwenyewe.
Kwa Viwango vya Jumuiya vifuatavyo, tunahitaji maelezo ya ziada na/au muktadha ili kutekeleza:
- Maonyesho ya Watu Binafsi na Vifaa vya Matibabu, yanayofafanuliwa kuwa maudhui yanayoonyesha mtu binafsi katika kituo cha matibabu au kituo cha afya au mtu binafsi au mtoto anayeingia au kutoka katika kituo cha matibabu au kituo cha afya, na yanaripotiwa na:
- Mtu aliye kwenye taswira
- Mwakilishi wa mtu aliye kwenye taswira
- Kituo cha matibabu au cha afya chenye majukumu ya kumtunza mtu aliye kwenye taswira, au
- Kituo cha matibabu au cha afya ambacho kimeajiri mtu aliye kwenye taswira
- Nyenzo asilia ambazo zinalenga kufichua maelezo yasiyo ya umma yanayohusiana na uchaguzi ulioshirikiwa kama sehemu ya operesheni ya ushawishi wa serikali ya kigeni.
- Tunaondoa kuripoti kuhusu uvujaji kama huo na vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali kutoka nchi iliyosababisha uvujaji huo.
Hali ya matumizi ya mtumiaji
Tazama mifano kadhaa ya jinsi utekelezaji unavyoonekana kwa watu kwenye Facebook, kama vile: inavyoonekana kuripoti kitu ambacho unafikiri hakipaswi kuwa kwenye Facebook, kuambiwa kuwa umekiuka Viwango vyetu vya Jumuiya na kuona skrini ya onyo juu ya maudhui fulani.
Dokezo: Tunaendelea kuboresha, kwa hivyo kile unachokiona hapa kinaweza kupitwa na wakati kiasi ikilinganishwa na kile tunachotumia sasa.
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Kuripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Mawasiliano ya baada ya ripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Hali ya kuondoa
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Skrini za onyo
Utekelezaji
Tuna sera sawa ulimwenguni kote, kwa ajili ya kila mtu kwenye Facebook.
Timu za ukaguzi
Timu yetu ya kimataifa ya wakaguzi zaidi ya 15,000 hufanya kazi kila siku kuweka watu kwenye Facebook kuwa salama.
Ushiriki wa mshikadau
Wataalamu wa nje, wasomi, mashirika yasiyo ya faida na watungaji sera husaidia kuweka Viwango vya Jumuiya ya Facebook.
Pata usaidizi wa ukiukaji wa faragha
Jifunze unachoweza kufanya ukiona kitu kwenye Facebook ambacho kinakiuka Viwango vyetu vya Jumuiya.
Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi