Taarifa isiyofaa

Maelezo ya sera

BADILISHA KUMBUKUMBU
Utaratibu wa Sera
Taarifa isiyofaa ni tofauti na aina nyingine ya usemi iliyoangaziwa katika Viwango vyetu vya Jumuiya kwa sababu hakuna njia ya kupambanua orodha tondoti ya kile kilichopigwa marufuku. Ukichukulia vurugu vya picha au maudhui ya chuki, kwa mfano, sera zetu zinabainisha maudhui ambayo tumeyapiga marufuku na hata watu ambao hawakubaliani na sera hizo wanaweza kuzifuata. Hata hivyo, kwa taarifa isiyofaa, hatuwezi kutoa tofauti kama hiyo. Dunia inabadilika kila mara na kilicho ukweli dakika moja huenda kisiwe ukweli dakika inayofuata. Watu wana viwango tofauti vya taarifa kuhusu ulimwengu karibu nao na wanaweza kuamini kuwa jambo fulani ni ukweli wakati sio. Sera ambayo inapiga tu marufuku “taarifa isiyofaa” huenda isitoe ilani muhimu kwa watu wanaotumia huduma zetu na huenda isiweze kutekelezwa, kwa kuwa hatuna ufikiaji kamili wa taarifa.
Badala yake, sera zetu zinafafanua kategoria tofauti za taarifa isiyofaa na kujaribu kutoa mwongozo wa wazi kuhusu jinsi tunavyoshughulikia usemi huo tunapouona. Kwa kila kategoria, mbinu yetu inaakisi juhudi zetu za kusawazisha maadili yetu ya kujieleza, usalama, hadhi, uhalali na faragha.
Tunaondoa taarifa isiyofaa pale ambapo ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari kutokea madhara ya kimwili. Pia tunaondoa maudhui yaliyo na uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa uingiliaji wa utendaji wa michakato ya kisiasa. Katika kubaini kile kinachoainishwa kama taarifa isiyofaa katika kategoria hizi, tunashirikiana na wataalamu huru walio na maarifa na ujuzi wa kutathmini ukweli wa maudhui na iwapo yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya kutokea madhara ya kimwili. Hii inajumuisha, kwa mfano, kushirikiana na mashirika ya haki za binadamu yanayopatikana mashinani katika nchi ili kubaini ukweli wa fununu kuhusu mgogoro wa kiraia.
Kwa taarifa nyingine yote isiyofaa, tunalenga kupunguza kipimo chake au kuunda mazingira yanayohimiza mazungumzo yenye manufaa. Tunajua kwamba watu mara nyingi hutumia taarifa isiyofaa katika njia zisizo na madhara, kama vile kutia chuku kwa hoja fulani (“Timu hii ina rekodi mbaya zaidi katika historia ya spoti hii”) au katika ucheshi au kejeli (“Mume wangu ameshinda tuzo ya Mume wa Mwaka.”) Wanaweza pia kushiriki uzoefu wao kupitia hadithi zilizo na mambo yasiyo sahihi. Katika visa fulani, watu wanashiriki maoni yao ya dhati ambayo wengine wanazingatia kuwa uwongo au kushiriki taarifa ambayo wanaamini kuwa ukweli lakini wengine wanazingatia kutokuwa kamilifu au kupotosha.
Kutambua jinsi ambavyo usemi huo ulivyo wa kawaida, tunalenga kuwapa watumiaji maelezo muhimu wakati kuna maudhui yenye uwezekano wa kupotosha au kukanganya. Kama sehemu ya juhudi hiyo, nje ye Marekani tunashirikiana na mashirika ya wahusika wengine ya ukaguzi wa ukweli katika sehemu kadhaa za dunia kukagua na kukadiria usahihi wa maudhui yanayovuma sana kwenye majukwaa yetu (tazama hapa na hapa ili kupata mtazamo wetu nchini Marekani). Kuanzia Marekani, mpango wa Madokezo ya Jumuiya huwezesha watu kuongeza muktadha zaidi kwenye machapisho ya Facebook, Instagram na Threads ambayo yana uwezekano wa kupotosha au kuchanganya (tazama hapa). Pia tunatoa rasilimali za kuongeza ujuzi wa kutumia midia na maudhui dijitali ili watu waweze kuamua kusoma, kuamini na kushiriki wenyewe. Tunataka watu wafichue, kwa kutumia zana inayotumia AI, kila wanapochapisha maudhui ya kikaboni yenye video za uhalisia wa picha au sauti zinazosikika kuwa halisi ambayo iliundwa au kubadilishwa kidijitali na tunaweza kuweka adhabu ikiwa watakosa kufanya hivyo. Pia tunaweza kuongeza lebo kwenye maudhui maalum yaliyoundwa au kubadilishwa kidijitali yanayounda hususan hatari kubwa ya kupotosha watu kuhusu masuala yenye umuhimu kwa umma.
Hatimaye, tunapiga marufuku maudhui na mwenendo katika nyanja nyingine ambayo mara nyingi hulandana na maenezi ya taarifa isiyofaa. Kwa mfano, Viwango vyetu vya Jumuiya vimepiga marufuku akaunti ghushi, udanganyifu na mwenendo unaoratibiwa usio halali.
Kadri mazingira ya mtandaoni na nje ya mtandao yanavyobadilika na kukua, ndivyo tunavyoendelea kukuza sera hizi. Akaunti ambazo zinashiriki kwa kurudia taarifa isiyofaa iliyoorodheshwa hapo chini zinaweza, pamoja na kutekelezwa kwa maudhui kwa mujibu wa sera hii, zinaweza kuwekewa vikomo kwa uwezo wao wa kutangaza au kuondolewa kwenye majukwaa yetu. Taarifa za ziada kuhusu kinachofanyika wakati Meta imeondoa maudhui inaweza kupatikana hapa.
Miongozo
Taarifa isiyofaa tunayoondoa:
Tunaondoa aina zifuatazo za taarifa isiyofaa:
I. Madhara ya Kimwili au Vurugu
Tunaondoa taarifa isiyofaa au uvumi ambao hauwezi kuthibitishwa ambao washirika wataalamu wamebaini kuwa na uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya kutokea kwa vurugu au madhara ya kimwili kwa watu. Tunafafanua taarifa isiyofaa kama maudhui yaliyo na dai ambalo limebainiwa kuwa la uwongo kupitia mhusika mwingine mwenye mamlaka. Tunafafanua uvumi ambao hauwezi kuthibitishwa kama dai ambalo chanzo kimethibitishwa na washirika wataalamu kuwa ni vigumu au hakiwezi kufuatiliwa, au ambao vyanzo vyao halali havipo, pale ambapo hakuna maelezo mahususi ya kuwewezesha dai kupuuziliwa, au pale ambapo dai halina msingi wowote au halina mantiki yoyote hivyo haliwezi kuaminika.
Tunafahamu kwamba wakati mwingine taarifa isiyofaa ambayo huenda ikaonekana kuwa ya ukarimu inaweza, katika muktadha mahususi, kuchangia kwa hatari ya madhara ya nje ya mtandao, ikijumuisha matishio ya vurugu yanayoweza kuchangia kwa hatari ya juu ya vifo, majeraha mabaya au madhara mengine ya kimwili. Tunafanya kazi na mtandao wa kimataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), mashirika yasiyo ya faida, mashirika ya kibinadamu na mashirika ya kimataifa yaliyo na wataalamu katika mabadiliko haya ya kindani.
Katika nchi ambazo zinakabiliwa na hatari kubwa ya vurugu ya kijamii, tunafanya kazi kwa bidii na washirika wa ndani kuelewa ni madai gani ya uwongo yanaweza kuchangia moja kwa moja hatari ya madhara ya mwili. Kisha tunajitahidi kutambua na kuondoa maudhui yanayotoa madai hayo kwenye mfumo wetu. Kwa mfano, kwa kushauriana na wataalamu wa eneo lako, tunaweza kuondoa maudhui yasiyo ya muktadha yanayodai kwa uwongo kuonyesha vitendo vya vurugu, wahasiriwa au wahusika wa vurugu, silaha au vifaa vya kijeshi.
II. Taarifa isiyofaa yenye Madhara Inayohusu Afya
Tunashauriana na mashirika yanayoongoza ya afya kutambua taarifa isiyofaa kuhusu afya ambayo ina uwezekano wa kuchangia kwa madhara kwa afya na usalama wa umma. Taarifa isiyofaa yenye madhara inayohusu afya ambayo tunaondoa inajumuisha:
  • Taarifa isiyofaa kuhusu chanjo. Tunaondoa taarifa isiyofaa kimsingi kuhusu chanjo wakati mamlaka za afya ya umma zimeamua kuwa taarifa ni ya uwongo na ina uwezekano wa kuchangia uwezekano wa watu kukataa chanjo. Hizi ni pamoja na:
    • Chanjo zinasababisha ugonjwa wa tawahudi (Mfano: “Kuongezeka kwa chanjo ndiyo sababu watoto wengi wanaugua tawahudi siku hizi.”)
    • Chanjo husababisha Vifo vya Ghafla vya Watoto Wadogo (Mf: “Je, hujui kwamba chanjo husababisha SIDS?”
    • Chanjo husababisha ugonjwa ambao zinapaswa kuponya, au kusababisha mtu anayepokea chanjo hiyo kuwa katika hatari ya juu ya kupata ugonjwa (Mfano: “Kupata chanjo kunakufanya kuwa katika hatari ya juu zaidi ya kupata ugonjwa kwa vile kuna chembechembe za ugonjwa ndani yake. Makinika!”)
    • Chanjo au viambato vyao vinauwa, ni sumu, vinadhuru au ni hatari (Mfano: “Hakika, unaweza kupata chanjo, ikiwa huna wasiwasi wa kuingiza sumu mwilini mwako.”)
    • Kingamwili asilia ni salama kuliko chanjo ya kupewa (Mfano: “Ni salama zaidi kupata ugonjwa wenyewe badala ya chanjo.”)
    • Ni hatari kupata chanjo kadhaa katika muda mfupi, hata kama muda huo umependekezwa kimatibabu (Mfano: “Usichukue zaidi ya chanjo moja kwa wakati mmoja, hiyo ni hatari - Sijali ni nini daktari wako atakuambia!”)
    • Chanjo si faafu katika kuzuia ugonjwa ambao zinatarajiwa kulinda dhidi yake. Hata hivyo, kwa chanjo za COVID-19, mafua na malaria, hatuondoi madai kwamba chanjo hizo si faafu katika kuzuia mtu kuambukizwa na virusi hivyo. (Mfano: Ondoa – “Chanjo ya polio haifanyi chochote kukukinga dhidi ya kupata ugonjwa”, Ondoa – “Kwa hakika chanjo hazifanyi chochote kukukinga dhidi ya kupata ugonjwa”, Ruhusu – “Chanjo haikuzuii kupata COVID-19, ndiyo sababu bado unahitaji kujitenga na watu na kuvaa barakoa unapokuwa karibu na wengine.”)
    • Kupewa ukambi hakuwezi kusababisha kifo (inahitaji taarifa zaidi na/muktadha) (Mfano: “Usiwe na wasiwasi kuhusu iwapo utapata ukambi, haiwezi kukuuwa.”)
    • Vitamini C inafaa tu kama chanjo inavyofaa katika kuzuia magonjwa ambayo chanjo zao zipo.
  • Taarifa isiyofaa kuhusu afya wakati wa dharura za afya ya umma. Tunaondoa taarifa isiyofaa nyakati za dharura za afya ya umma wakati mamlaka za afya ya umma zimehitimisha kwamba taarifa hiyo ni ya uwongo na ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya kutokea kwa madhara ya kimwili, ikijumuisha kwa kuchangia kwa hatari ya watu binafsi kupata au kueneza ugonjwa hatari au kukataa chanjo husiani. Tunatambua dharura za afya ya umma kwa ushirikiano na mamlaka za kimataifa na ndani za afya.
  • Kutangaza au kutetea tiba za kimiujiza zenye madhara kwa matatizo ya afya. Hii inajumuisha matibabu ambapo matumizi yanayopendekezwa, katika muktadha wa afya, yana uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa majeraha mabaya ya kimwili au kifo, na tiba haina matumizi halali ya afya (mfano: kuchubua ngozi, dawa ya kuua viini, black salve/tiba ya saratani, caustic soda).
III. Kuingilia Upigaji Kura au Sensa
Katika juhudi za kuhimiza uadilifu wa uchaguzi na sensa, tunaondoa taarifa isiyofaa ambayo ina uwezekano wa kuchangia moja kwa moja kwa hatari ya kuingilia uwezo wa watu kushiriki kwenye michakato hiyo. Hii inajumuisha yafuatayo:
  • Taarifa isiyofaa kuhusu tarehe, maeneo, saa na mbinu za kupiga kura, usajili wa wapiga kura au kushiriki kwenye sensa.
  • Taarifa isiyofaa kuhusu ni nani aliyehitimu kupiga kura, mahitaji ya kuhitimu kupiga kura, ikiwa kura itahesabiwa na ni maelezo yepi na vifaa ambavyo lazima ziwasilishwe ili kuweza kupiga kura.
  • Taarifa isiyofaa kuhusu iwapo mwaniaji anagombea kiti au la.
  • Taarifa isiyofaa kuhusu anayeweza kushiriki kwenye sensa na taarifa au vifaa ambavyo ni lazima atoe ili aweze kushiriki.
  • Taarifa isiyofaa kuhusu kuhusika kwa serikali katika sensa, ikiwa ni pamoja,ambapo inahitajika, kwamba taarifa ya sensa ya mtu binafsi itashirikiwa na shirika jingine la serikali (isiyo ya sensa).
  • Madai ya uwongo au yasiyothibitishwa kwamba Taasisi ya Kutekeleza Uhamiaji na Forodha nchini Marekani (ICE) ipo katika eneo la upigaji kura
  • Madai wazi ya uwongo kwamba watu wataambukizwa COVID-19 (au magonjwa mengine ya kuambukiza) ikiwa watashiriki katika mchakato wa kupiga kura.
  • Madai ya uwongo kuhusu hali za sasa katika eneo la kupigia kura Marekani ambazo zitafanya iwe vigumu kupiga kura, kama ilivyothibitishwa na halmashauri ya kusimamia uchaguzi.
Tuna sera za ziada zinazonuiwa kushughulikia miito ya virugu, kuendeleza kushiriki kwa njia haramu, na miito ya uingiliaji ulioratibiwa wa uchaguzi, ambazo zinawakilishwa katika sehemu nyingine ya Viwango vyetu vya Jumuiya.
Kwa maudhui yafuatayo, tunajumuisha lebo ya maelezo:
Midia Iliyobadilishwa
Midia inaweza kuhaririwa kwa njia mbalimbali. Katika visa vingi, mabadiliko haya hayana madhara, kama vile maudhui kukuzwa au kufupishwa kwa sababu za kisanii au kuongezewa muziki. Katika visa vingine, mabadiliko hayo si wazi na yanaweza kupotosha.
  • Maudhui Yaliyoundwa au Kubalishwa Kidijitali yanayoweza Kupotosha. Kwa maudhui ambayo vinginevyo yanakiuka Viwango vya Jumuiya, tunaweza kuweka lebo ya maelezo kwenye kiini cha maudhui – au kukataa maudhui yaliyowasilishwa kama tangazo – wakati maudhui yana picha au video za uhalisia, au sauti ya uhalisia, iliyoundwa au kubadilishwa kidijitali na kuunda hususani hatari kubwa ya nyenzo zinazodanganya umma kuhusu masuala ya umuhimu wa umma.
Hali ya matumizi ya mtumiaji
Tazama mifano kadhaa ya jinsi utekelezaji unavyoonekana kwa watu kwenye Facebook, kama vile: inavyoonekana kuripoti kitu ambacho unafikiri hakipaswi kuwa kwenye Facebook, kuambiwa kuwa umekiuka Viwango vyetu vya Jumuiya na kuona skrini ya onyo juu ya maudhui fulani.
Dokezo: Tunaendelea kuboresha, kwa hivyo kile unachokiona hapa kinaweza kupitwa na wakati kiasi ikilinganishwa na kile tunachotumia sasa.
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Kuripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Mawasiliano ya baada ya ripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Hali ya kuondoa
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Skrini za onyo
Utekelezaji
Tuna sera sawa ulimwenguni kote, kwa ajili ya kila mtu kwenye Facebook.
Timu za ukaguzi
Timu yetu ya kimataifa ya wakaguzi zaidi ya 15,000 hufanya kazi kila siku kuweka watu kwenye Facebook kuwa salama.
Ushiriki wa mshikadau
Wataalamu wa nje, wasomi, mashirika yasiyo ya faida na watungaji sera husaidia kuweka Viwango vya Jumuiya ya Facebook.
Pata usaidizi wa taarifa isiyofaa
Jifunze unachoweza kufanya ukiona kitu kwenye Facebook ambacho kinakiuka Viwango vyetu vya Jumuiya.
Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi