Katika juhudi za kuvuruga na kuzuia, tunaondoa maudhui ambayo husaidia au kuratibu matumizi mabaya ya binadamu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa binadamu. Tunafafanua usafirishaji wa binadamu kuwa biashara ya kumnyima mtu uhuru wa kupata faida. Ni matumizi mabaya ya binadamu ili kuwalazimisha kujihusisha katika biashara ya ngono, kazi au shughuli nyingine dhidi ya matakwa yao. Hutegemea udanganyifu, matumizi ya mabavu, na kulazimishwa na hushusha thamani ya binadamu kwa kuwanyima uhuru wao huku watu wengine wakinufaika kiuchumi na mali.
Usafirishaji wa binadamu ni tukio la namna nyingi na hutokea ulimwenguni kote; huweza kuathiri mtu yoyote licha ya umri, usuli wa kiuchumi na jamii, kabila, jinsia au eneo. Hufanyika kwa namna nyingi na hali yoyote ile ya usafirishaji unaweza kuhusisha hatua mbalimbali za ukuaji. Kutokana na hali ya kulazimishwa kwa matumizi haya mabaya, waathiriwa hawawezi kutoa idhini.
Huku tukihitajika kuwa kamili ili tusichanganye usafirishaji wa binadamu na magendo, yanaweza kuwa na uhusiano na kuonyesha kulandana. Umoja wa Mataifa unafafanua magendo ya binadamu kuwa utaratibu wa kusaidia mtu kuingia kimagendo katika nchi kupitia mipaka ya kimataifa. Bila umuhimu wa kulazimisha au kutumia mabavu, bado inaweza kusababisja matumizi mabaya ya watu walio hatarini ambao wanajaribu kuondoka nchini kwao asili, mara nyingi kwa kufuata maisha bora. Magendo ya binadamu ni uhalifu dhidi ya nchi, kutegemea safari na usafirishaji wa binadamu ni uhalifu dhidi ya mtu, anayetegemea matumizi mabaya.
Kando na maudhui yanayokashifu, kutoa uhamasisho kuhusu, au kuripoti habari kuhusu masuala ya biashara ya usafirishaji wa binadamu au magendo ya binadamu, tunaruhusu maudhui yanayoomba au kushiriki maelezo kuhusu usalama wa kibinafsi na kuvuka mpakani, kutafuta usalama katika nchi ya nje au jinsi ya kuondoka katika nchi fulani.
Usichapishe:
Maudhui, shughuli aua miingiliano inayosajili watu, kuwezesha au kunyanyasa watu kupitia namna yoyote ya biashara ya usafirishaji wa binadamu:
Biashara haramu ya ngono (shughuli yoyote ya kibiashara ya ngono inayohusu mtoto mdogo au shughuli yoyote ya kibiashara ya ngono inayohusu mtu mzima ambayo inahusisha nguvu, ulaghai au kushurutisha)
Mauzo ya watoto au upangaji usio halali
Ulanguzi wa mayatima na utalii wa mayatima
Ndoa za lazima (ikiwa ni pamoja na ndoa zinazohusisha watoto)
Matumizi mabaya kikazi (ikiwa ni pamoja na kazi za mateka)
Utumwa wa nyumbani
Biashara ya viungo vya mwili isiyo ya kurudia, bila kujumuisha kuondoa viungo, michango au upandikizaji katika muktadha wa mchango wa kiungo usio wa unyanyasaji
Shughuli za kulzimishwa za jinai (k.m kulazimisha mtu kuwa mwombaji, kulazimisha mtu kuwa mlanguzi wa dawa)
Kusajili watoto kuwa wanajeshi
Maudhui ambapo mtendaji mwingine huajiri, kuwezesha au kufaidika na (kifedha au njia nyinginezo) shughuli za kibiashara za ngono.
Maudhui ambayo hutoa kutoa au kuwezesha ulanguzi wa binadamu
Maudhui yanayoomba huduma za ulanguzi wa binadamu
Tunaruhusu maudhui ambayo yanashughulikiwa vinginevyo na sera hii yanapochapishwa katika miktadha ya kulaani, kuelimisha, kutoa uhamasisho, au kuripoti habari.
Chini ya sera zetu za Unyanyasaji wa Binadamu, wakaguzi wetu na mifumo otomatiki pia inaweza kuzingatia ishara mbalimbali za kitabia ili kusaidia kugundua na kuchukua hatua kuhusu akaunti zinazokiuka.
- Tunaweza kuondoa akaunti kulingana na mwingiliano wao na akaunti nyingine zinazokiuka, utafutaji au mwingiliano na maudhui yanayokiuka, au uanachama katika jumuiya (k.m Vikundi) ambavyo tumeondoa kwa kukiuka sera zetu.
Kwa Viwango vya Jumuiya vifuatavyo, tunahitaji maelezo ya ziada na/au muktadha ili kutekeleza: