Watu Binafsi na Mashirika Hatari

Maelezo ya sera

BADILISHA KUMBUKUMBU
Utaratibu wa Sera
Katika juhudi za kuzuia na kuharibu madhara katika ulimwengu halisi, haturuhusu mashirika au mtu binafsi anayedai misheni ya vurugu au anayejihusisha katika vurugu kuwa na uwepo kwenye majukwaa yetu. Tunatathmini mashirika haya kulingana na tabia zao mtandaoni na nje ya mtandao, kwa umuhimu zaidi, uhusiano wao na vurugu. Chini ya sera hii, tunabainisha watu, mashirika, na mitandao ya watu. Majina haya yamegawanywa katika viwango viwili vinavyoonyesha kiwango cha utekelezaji wa maudhui, na Ngazi ya 1 ikisababisha utekelezaji wa kina zaidi kwa sababu tunaamini mashirika haya yana uhusiano wa moja kwa moja na madhara ya nje ya mtandao.
Ngazi ya 1 inaangazia mashirika yanayojihusisha na madhara mabaya ya nje ya mtandao - ikiwemo kupanga au kutetea vurugu dhidi ya raia, udhalilishaji wa kurudia au kutetea madhara dhidi ya watu kulingana na sifa zilizolindwa, au kushiriki katika operesheni za kihalifu za kimfumo. Ngazi ya 1 inajumuisha mashirika ya chuki; mashirika ya uhalifu, pamoja na yale yaliyoteuliwa na serikali ya Marekani Kama Wafanyabiashara Maalum wa Biashara ya Dawa za Kulevya (SDNTKs); na mashirika ya kigaidi, pamoja na mashirika na watu binafsi walioteuliwa na serikali ya Marekani kama Mashirika ya Kigaidi ya Kigeni (FTOs) au Magaidi Maalum Walioteuliwa Ulimwenguni (SDGTs). Tunaondoa Utukuzo Uungaji Mkono, na Uwakilishi wa shirika lililo katika Ngazi ya 1, viongozi wao, waanzilishi au wanachama wao mashuhuri, pamoja na marejeo yasiyo wazi kwao.
Kando na hayo, haturuhusu maudhui yanayotukuza, kuunga mkono, au kuwakilisha matukio ambayo Meta imebainisha kama matukio ya vurugu ya ukiukaji - ikiwemo mashambulizi ya kigaidi, matukio ya chuki, vurugu kwa waathiriwa wengi au jaribio la vurugu kwa waathiriwa wengi, mauaji ya mfuatano, au uhalifu wa chuki. Wala haturuhusu (1) Utukuzo, Uungaji mkono, au Uwakilishi wa wahusika wa katika mashambulizi kama hayo. (2) maudhui yanayotokana na wahalifu ambayo yanahusiana na mashambulizi kama hayo; au (3) taswira ya wahusika wengine inayoonyesha wakati wa shambulio kama hilo ya waathiriwa wanaoonekana. Pia tunaondoa maudhui ambayo Yanatukuza, Kuunga mkono au Kuwakilisha itikadi zinazoendeleza chuki, kama vile unazi na mamlaka ya watu weupe. Tunaondoa marejeleo yasiyo wazi ya matukio au itikadi hizi zilizoteuliwa.
Ngazi ya 2 inajumuisha Watendaji Wenye Vurugu Wasio wa Kiserikali ambao wanaojihusisha na vurugu dhidi ya watendaji wa serikali au wanajeshi katika mzozo wa silaha lakini hawalengi raia kimakusudi. Pia inajumuisha Mashirika Yanayochochea Vurugu ambayo yanajishughulisha na kuandaa au kutetea vurugu baadaye lakini hayajihusishi na vurugu hadi sasa. Haya pia ni mashirika ambayo yanaweza kujihusisha mara kwa mara katika ukiukaji wa sera zetu za Mwenendo wa Chuki au Mashirika na Watu Binafsi Hatari kwenye au nje ya jukwaa. Tunaondoa Utukuzo, Uungaji Mkono, na Uwakilishi wa mashirika haya, viongozi wao, waanzilishi au wanachama wao mashuhuri.
Tunatambua kuwa watumiaji wanaweza kushiriki maudhui yanayojumuisha marejeleo kwa mashirika na watu binafsi hatari katika muktadha wa mijadala ya kijamii na kisiasa. Hii inajumuisha kuripoti maudhui, kujadili bila upendeleo wowote au kushutumu mashirika na watu binafsi hatari au shughuli zao.
Kuripoti habari kunajumuisha maelezo yanayoweza kushirikiwa ili kutoa uhamasisho kuhusu matukio ya eneo na ya kimataifa ambayo watu binafsi na mashirika yaliyobainishwa kuwa hatari yanahusika.
  • K.m. “Habari za Hivi Punde: Al-Shabab walidai kuhusika katika shambulizi nchini Somalia”
  • K.m. “Kalenda ya matukio na uchanganuzi wa mtaalamu: Jinsi tukio la ufyatulianaji risasi katika Duka Kubwa la Buffalo lilivyofanyika na kile wahusika walisema mahakamani”
Majadiliano yasiyoegemea upande wowote inajumisha taarifa za kweli, maoni, maswali na taarifa nyingine ambayo hayaonyeshi hukumu chanya ya moja kwa moja kuhusu watu binafsi na mashirika yaliyobainishwa na tabia zao.
  • K.m. “Al Qaeda inawakilisha tishio ndogo kuliko ISIS kutokana na kukosa uongozi na ufadhili”
  • K.m. “Anders Breivik ni mojawapo ya mifano ya jinsi mchakato wa siasa kali unavyoweza kuwa changamano”
Kukashifu, ni pamoja na kutoidhinisha, kukereka, kukataa, kusuta, kudhihaki na semi nyingine hasi kuhusu watu binafsi na mashirika yaliyobainishwa kuwa hatari na tabia zao.
  • K.m. “Ninahisi kukerwa na uhalifu wa Salvador Ramos. Maneno ya hakimu yaliendana sana na hisia zangu. Hapaswi kuonewa huruma na mahakama”
  • K.m. “Uhalifu wa Hitler hautawai kusahaulika kamwe. Haya yalikuwa baadhi ya matukio mabaya zaidi katika historia”
Sera zetu zimeundwa ili “kuruhusu nafasi kwa aina hizi za majadiliano wakati huohuo ikipunguza hatari za madhara yanayoweza kutokea nje ya mtandao.” Kwa hivyo, Meta tunahitaji “watu waonyeshe wazi nia yao wanapounda au kushiriki maudhui kama hayo. Ikiwa nia ya mtumiaji haieleweki au si wazi, tunaondoa maudhui kwa chaguo-msingi.
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu, sera zetu huruhusu majadiliano kuhusu haki za binadamu za watu walioteuliwa au wanachama wa taasisi hatari zilizoteuliwa, isipokuwa maudhui yanajumuisha utukuzo, uungaji mkono, au uwakilishi wa mashirika yaliyoteuliwa au ukiukaji mwingine wa sera, kama vile uchochezi wa vurugu.
Tafadhali tazama Sera ya Haki za Binadamu za Shirika kwa maelezo zaidi kuhusu ahadi zetu kwa haki za binadamu zinazotambulika kimataifa.
Tunaondoa:
Tunaondoa Utukuzo, Uungaji Mkono, na Uwakilishi wa watu binafsi na mashirika mbalimbali hatari. Dhana hizi zinatumika kwa mashirika yenyewe, shughuli zao, na wanachama wao. Dhana hizi hazikatazi utetezi wa amani kwa ajili ya matokeo fulani ya kisiasa.
Utukuzo, hufafanuliwa kama yoyote yaliyo hapa chini:
  • Uhalalishaji au utetezi wa vitendo vya vurugu au vya chuki vya shirika lililobainishwa kwa kudai kuwa vitendo hivyo vina misingi ya kimaadili, kisiasa, kimantiki au sababu nyingine zinazozifanya kukubalika au kufaa.
    • K.m. “Hitler hakufanya chochote kibaya.”
  • Kusifu au kusherehekea vurugu au chuki dhidi ya shirika lililobainishwa kama ni mafanikio au ufanisi;
    • K.m. “Hizbul Mujahideen anashinda vita vya kupigania uhuru na kujisimimamia kwa Kashmir”
  • Taarifa ya matamanio ya kuwa na uanachama au taarifa kwamba ungependa kuwa shirika lililobainishwa au anayeendeleza tukio la ukiukaji la vurugu.
    • K.m. “Natamani ningeweza kujiunga na ISIS na niwe sehemu ya Khilafah”
Tunaondoa Utukuzo wa shirika la Ngazi ya 1 na Ngazi ya 2 na pia matukio yaliyoteuliwa.
Kwa Ngazi ya 1 na matukio yaliyoteuliwa, tunaweza pia kuondoa marejeleo yasiyoeleweka au yasiyo na muktadha ikiwa nia ya mtumiaji haikuonyeshwa wazi. Hii inajumuisha ucheshi usio wazi, marejeleo yasiyo na manukuu au chanya ambayo hayatukuzi vurugu au chuki ya shirika lililoteuliwa.
Uungaji mkono, hufafanuliwa kama yoyote yaliyo hapa chini:
  • Msaada wa Nyenzo
    • Kitendo chochote ambacho kinaboresha hali ya kifedha ya shirika lililoteuliwa – pamoja na kutoa pesa kwa ajili ya au kwenye shirika lililoteuliwa;
      • K.m., “Changia KKK!”
    • Kitendo chochote ambacho hutoa msaada mkubwa kwa shirika au tukio lililoteuliwa;
      • K.m., “Ikiwa unataka kutuma vifurushi vya huduma kwa Sinaloa Cartel, tumia anwani hii:”
    • Kuajiri kwa niaba ya shirika au tukio lililoteuliwa;
      • K.m., “Ikiwa unataka kupigania Caliphate, nitumie ujumbe wa moja kwa moja”
  • Msaada Mwingine
    • Kutoa taarifa au rasilimali, ikiwa ni pamoja na mawasiliano rasmi, kwa niaba ya shirika au tukio lililoteuliwa
      • K.m., Kunukuu moja kwa moja shirika lililoteuliwa bila manukuu yanayolaani, kujadili bila kuegemea upande wowote, au ni sehemu ya kuripoti habari.
    • Kutoa mwito wa hatua kwa niaba ya shirika au tukio lililoteuliwa;
      • K.m. “Wasiliana na Divisheni ya Atomwaffen – (XXX) XXX-XXXX”
Tunaondoa Usaidizi wote wa Ngazi ya 1 na Msaada wa Nyenzo wa Ngazi ya 2.
Uwakilishi, hufafanuliwa kama yoyote yaliyo hapa chini:
  • Kusema kwamba wewe ni mwanachama wa shirika lililoteuliwa, au ni shirika lililoteuliwa;
    • K.m, “Mimi ni joka kubwa la KKK.”
  • Kuunda Ukurasa, Wasifu, Tukio, Kikundi, au shirika lingine la Facebook ambalo ni au linalodai kuwa linamilikiwa na Shirika Lililoteuliwa au linaendeshwa kwa niaba yao, au ni au linadai kuwa tukio lililoteuliwa.
    • K.m., Ukurasa ulioitwa “Chama cha Nazi cha Marekani.”
Tunaondoa Uwakilishi wa Mashirika Yaliyoteuliwa na matukio yaliyoteuliwa ya Ngazi ya 1 na 2.
Aina na Ngazi za Mashirika Hatari
Ngazi ya 1: Ugaidi, chuki iliyopangwa, shughuli ya uhalifu ya kiwango kikubwa, jaribio la vurugu kwa waathiriwa wengi, vurugu kwa waathiriwa wengi, mauwaji ya mfuatano na matukio ya vurugu ya ukiukaji
Haturuhusu watu binafsi au mashirika yanayohusika na uhalifu uliopangwa, ikiwa ni pamoja na yale yaliyoteuliwa na serikali ya Marekani kama wafanyabiashara maalum wa biashara ya dawa za kulevya (SDNTKs); chuki; au ugaidi, pamoja na mashirika yaliyoteuliwa na serikali ya Marekani kama Mashirika ya Kigaidi ya Kigeni (FTOs) au Magaidi Maalum Walioteuliwa Ulimwenguni (SDGTs), kuwa kwenye jukwaa. Pia haturuhusu watu wengine kuwakilisha mashirika haya. Haturuhusu viongozi au wanachama mashuhuri wa mashirika haya kuwa na nafasi kwenye jukwaa, alama zinazowawakilisha kutumika kwenye jukwaa, au maudhui yanayowatukuza au matendo yao, ikijumuisha marejeleo yasiyoeleweka kwao. Kwa kuongeza, tunaondoa aina yoyote ya kuunga mkono watu binafsi na mashirika haya.
Haturuhusu maudhui yanayotukuza, kuunga mkono, au kuwakilisha matukio ambayo Meta imebainisha kama mashabulizi ya kigaidi ikiwemo mashambulizi ya kigaidi, matukio ya chuki, vurugu kwa waathiriwa wengi au jaribio la vurugu kwa waathiriwa wengi, mauaji ya mfuatano, uhalifu wa chuki au matukio ya vurugu ya ukiukaji. Wala haturuhusu (1) maudhui yanayotukuza, kuunga mkono, au kuwakilisha wahusika wa mashambulizi kama hayo. (2) maudhui yanayotokana na wahalifu ambayo yanahusiana na mashambulizi kama hayo; au (3) taswira ya wahusika wengine inayoonyesha wakati wa shambulio kama hilo ya waathiriwa wanaoonekana.
Pia haturuhusu Utukuzo, Uungaji Mkono, au Uwakilishi wa itikadi zilizobainishwa za chuki, pamoja na marejeleo yasiyokuwa wazi.
Mashirika ya kigaidi na watu binafsi, wanaofafanuliwa kama mtendaji asiye wa serikali:
  • Hujihusisha, kupigania au kutoa msaada muhimu kwa matendo ya kudhamiriwa na yaliyopangwa ya vurugu,
  • Yanayosababisha au kujaribu kusababisha kifo, jeraha au madhara mabaya kwa raia, au mtu mwingine kutoshiriki moja kwa moja kwenye uadui katika hali ambapo kuna mgogoro wa kujiami, na/au uharibifu wa kiasi cha haja kwa mali inayohusishwa na kifo,majeraha mabaya au madhara mabaya kwa raia
  • Kwa nia ya kushurutisha, kushtua na/au kuchochea raia, serikali au shirika la kimataifa
  • Ili kufikia lengo la kisiasa, kidini, au la kiitikadi.
Shirika la Chuki, linafafanuliwa kama shirika au mtu binafsi anayeeneza na kuhimiza chuki dhidi ya wengine kulingana na sifa zao zinazolindwa. Shughuli za shirika hilo hubainishwa kwa angalau baadhi ya tabia zifuatazo:
  • Vurugu, matamshi ya kutisha, au aina hatari za unyanyasaji zinazolenga watu kulingana na sifa zao zinazolindwa;
  • Matumizi ya mara kwa mara ya matamshi ya chuki;
  • Uwakilishi wa Itikadi za Chuki au Mashirika mengine yaliyoteuliwa ya Chuki, na/au
  • Kutukuza au Kuunga mkono Mashirika mengine yaliyoteuliwa ya Chuki au Itikadi za Chuki.
Mashirika ya Jinai, hufafanuliwa kama ushirika wa watu watatu au zaidi ambao:
  • umeunganishwa kwa jina, rangi, ishara ya mikono au dalili inayotambuliwa; na
  • umehusika au unatishia kushiriki katika shughuli za jinai kama vile mauaji, usafirishaji wa mihadarati, au utekaji nyara.
Vurugu kwa Waathiriwa Wengi na Mauwaji ya Mfuatano
  • Tunazingatia tukio kuwa vurugu kwa waathiriwa wengi au jaribio la vurugu kwa waathiriwa wengi ikiwa itasababisha majeruhi ya watu watatu au zaidi katika tukio moja, linalofafanuliwa kama vifo au majeraha mabaya. Mtu yeyote ambaye amefanya shambulio kama hilo anazingatiwa kuwa mtuhumiwa au mtuhumiwa wa jaribio la vurugu kwa waathiriwa wengi.
  • Tunazingatia mtu aliyetekeleza mauwaji ya watu wawili au zaidi katika matukio au maeneo mengi kama muuwaji wa mfuatano.
Itikadi za Chuki
  • Ingawa uteuzi wetu wa mashirika na watu binafsi unazingatia tabia, tunatambua pia kuwa kuna itikadi na imani fulani ambazo asili yake zinahusiana na vurugu na kujaribu kupanga watu kuelekea wito wa vurugu au kutenga wengine kulingana na sifa zao zilizolindwa. Katika visa hivi, tunachagua itikadi yenyewe na kuondoa maudhui yanayounga mkono itikadi hii kutoka kwenye jukwaa letu. Itikadi hizi zinajumuisha:
    • Unazi
    • Mamlaka ya Wazungu
    • Utaifa wa Wazungu
    • Utengano wa Wazungu
  • Tunaondoa Utukuzaji, Uungaji Mkono, na Uwakilishi wazi wa itikadi hizi, na tunaondoa watu binafsi na mashirika ambayo yanaelezea moja au zaidi ya itikadi hizi za chuki.
Ngazi ya 2: Watendaji wa Vurugu Wasio wa Serikali na Mashirika Yanayochochea Vurugu
Mashirika na watu binafsi waliobainishwa na Meta kama Watendaji wa Vurugu Wasio wa Serikali au Mashirika Yanayochochea Vurugu hawaruhusiwi kuwa na nafasi kwenye Facebook, au kuwa na nafasi unaodumishwa na wengine kwa niaba yao. Kwa vile jumuiya hizi zinashiriki kikamilifu katika vurugu, dhidi ya watendaji wa serikali au kijeshi katika mizozo ya kivita (Watendaji wa Vurugu Wasio wa Serikali) au wanatayarisha au kutetea au kuunda mazingira ya vurugu za siku zijazo (Mashirika Yanayochochea Vurugu), msaada wa nyenzo wa mashirika haya hauruhusiwi. Pia tutaondoa utukuzo wa mashirika haya.
Watendaji wa Vurugu Wasio wa Serikali, inaelezewa kama mtendaji yeyote asiye wa serikali ambaye:
  • Hushiriki katika mtindo wa vitendo vilivyokusudiwa na vilivyopangwa vya vurugu la ubaya wa juu vinavyolenga serikali, wanajeshi au vikundi vingine vyenye silaha vinavyoshiriki moja kwa moja katika uhasama katika hali ya mapigano ya kivita, na havilengi kwa makusudi na kwa uwazi raia wenye vurugu la ubaya wa juu; NA/AU
  • Kunyima jamii uwezo wa kufikia miundomsingi muhimu au maliasili; NA/AU
  • Hujihusisha na mtindo wa mashambulizi yanayokusudiwa kuleta uharibifu mkubwa kwa miundombinu ambao hauhusiani na kifo, majeraha kali au madhara makubwa kwa raia.
Mashirika Yanayochochea Vurugu yanafafanuliwa kama ifuatavyo:
Shirika Linalochochea Vurugu (Jumla) ni mtendaji asiye wa serikali ambaye:
  • Ina lengo au jukumu lililokusudiwa kama ilivyoelezwa kutoa, kupitia vurugu, kazi ya utekelezaji wa serikali isiyoidhinishwa (kama vile, polisi, jeshi, uhamiaji) badala ya, au kwa kuongezea, serikali yenyewe; au kuvuruga kupita kukatiza jukumu la utekelezaji wa sheria la serikali;
  • Imechukua hatua kubwa kuelekea lengo hili lililotajwa kwenye majukwaa ya Meta; na
  • Imeshiriki katika visa vingi vya kutishia au kuchochea vurugu kali (mtandaoni au nje ya mtandao);
Shirika la Chuki Lililopigwa Marufuku ni mtendaji asiyekuwa wa serikali ambaye:
  • Hujihusisha na tabia ya kuchukiza mara kwa mara au yenye kutia madoido, lakini hafikii kiwango cha shirika la Ngazi ya 1 kwa sababu hawajashiriki au kutetea wazi vurugu, au kwa sababu hawana uhusiano wa kutosha wa mashirika au takwimu zilizoteuliwa hapo awali.
Kwa Viwango vya Jumuiya vifuatavyo, tunahitaji maelezo ya ziada na/au muktadha ili kutekeleza:
  • Katika kesi fulani, tutaruhusu maudhui ambayo vinginevyo yanaweza kukiuka Viwango vya Jumuiya inapobainika kwamba maudhui hayo ni ya tashtiti. Maudhui yataruhusiwa tu ikiwa vipengee vinavyokiuka vya maudhui hayo vimefanywa kama vya tashtiti au kuhusishwa na kitu au mtu ili kumdhihaki au kumsuta.
Hali ya matumizi ya mtumiaji
Tazama mifano kadhaa ya jinsi utekelezaji unavyoonekana kwa watu kwenye Facebook, kama vile: inavyoonekana kuripoti kitu ambacho unafikiri hakipaswi kuwa kwenye Facebook, kuambiwa kuwa umekiuka Viwango vyetu vya Jumuiya na kuona skrini ya onyo juu ya maudhui fulani.
Dokezo: Tunaendelea kuboresha, kwa hivyo kile unachokiona hapa kinaweza kupitwa na wakati kiasi ikilinganishwa na kile tunachotumia sasa.
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Kuripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Mawasiliano ya baada ya ripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Hali ya kuondoa
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Skrini za onyo
Data
Tazama Ripoti ya sasa ya Utekelezwaji wa Viwango vya Jumuiya
Utekelezaji
Tuna sera sawa ulimwenguni kote, kwa ajili ya kila mtu kwenye Facebook.
Timu za ukaguzi
Timu yetu ya kimataifa ya wakaguzi zaidi ya 15,000 hufanya kazi kila siku kuweka watu kwenye Facebook kuwa salama.
Ushiriki wa mshikadau
Wataalamu wa nje, wasomi, mashirika yasiyo ya faida na watungaji sera husaidia kuweka Viwango vya Jumuiya ya Facebook.
Pata usaidizi wa watu binafsi na mashirika hatari
Jifunze unachoweza kufanya ukiona kitu kwenye Facebook ambacho kinakiuka Viwango vyetu vya Jumuiya.
Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi