Utaratibu wa Sera
Tunatambua kwamba usalama wa watumiaji wetu unajumuisha usalama wa maelezo yao ya kibinafsi, akaunti, wasifu na majukwaa mengine tanzu ya Meta ambayo wanaweza kuwa wanadhibiti, pamoja na bidhaa na huduma zetu kwa upana zaidi. Majaribio ya kutaka kukusanya maelezo ya kibinafsi au kuhusishwa katika ufikiaji usioruhusiwa kupitia mbinu za uongo au uvamizi yana madhara kwa mazingira halisi, wazi na salama tunayotaka kuhimiza.
Haturuhusu:
Majaribio ya kuingilia au kufikia akaunti kupitia njia ambazo hazijaidhinishwa, ikiwa ni pamoja na:
Kufikia akaunti, wasifu au mashirika mengine ya Meta, tofauti na za mtu binafsi kupitia njia za udanganyifu au bila idhini ya moja kwa moja kutoka kwa mmiliki wa akaunti, wasifu au shirika.
Kupata, kununua au kuomba maelezo ya kuingia ya mtumiaji mwingine, taarifa binafsi au taarifa nyingine nyeti kwa madhumuni ya ufikiaji usioidhinishwa, ikiwa ni pamoja na kupitia mbinu zifuatazo:
Wizi wa data binafsi, inayofafanuliwa kama tabia ya kuunda mawasiliano au tovuti ambazo zimesanifiwa ili kufanana na mawasiliano au tovuti zinazoaminika au zenye hadhi zaidi kwa madhumuni ya kupata taarifa nyeti za mtumiaji kwa njia ya udanganyifu.
Kuwahadaa watu, kama vile kurudia au jaribio la mara kwa mara la kuvuna au kupata majibu ya kawaida ya maswali ya kurejesha akaunti au nenosiri.
Programu hasidi, Programu zisizotakikana, Vidadisi au misimbo mingine hasidi kama ilivyoelezwa hapa chini.
Majaribio ya kushiriki, kuunda, kupangisha au kusambaza msimbo hasidi au hatari, ikiwa ni pamoja na:
Kuhimiza au kuwahadaa watumiaji kupakua au kuendesha faili, programu au mipango ambayo itaingilia usalama wa data na uwepo wa mtumiaji mtandaoni, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:
Programu hasidi, inayofafanuliwa kama msimbo au programu iliyoundwa ili kudhuru au kupata ufikiaji usioidhinishwa wa mifumo. Hii ni pamoja na programu ambazo zimesanifiwa ili kudhuru mifumo ya kompyuta, pamoja na programu ziizosanifiwa ili kupata pesa kutoka kwa waathiriwa, kama vile programu ya kudai fidia ili kuachilia mateka.
Vidadisi, vinavyofafanuliwa kama msimbo au programu zinazokusanya data kuhusu watumiaji na kuituma kwa wahusika wengine bila idhini iliyofahamishwa ya mtumiaji, au inayotumia data kwa madhumuni haramu (m.f.,kuomba pesa kwa kutishia kuvuja picha nyeti, kuhadaa, ufikiaji haramu wa mifumo).
Programu isiyotakikana, inafafanuliwa kama msimbo au programu ambayo inazuia matumizi ya maunzi au programu na inayoweza kuwa vigumu kuondoa kwenye mtandao au mfumo wa kompyuta.
Kuunda, kushiriki au kupangisha programu hasidi ikiwemo viendelezi vya kivinjari na programu za vifaa vya mkononi, kwenye au nje ya jukwaa linaloweka watumiaji au bidhaa na huduma zetu hatarini.
Kutishia, kukubali au kuwezesha udukuzi - Ikiwa ni pamoja na kushiriki au kutangaza programu, kozi au bidhaa zinazowezesha watu kukwepa mifumo ya usalama, ikiwa ni pamoja na programu zinazohimiza uvamizi wa programu au stakabadhi
Kutoa miundomsingi mtandaoni, ikiwa ni pamoja na huduma za kupangisha wavuti, seva za mfumo za jina la kikoa na mitandao ya tangazo inayowezesha viungo vinavyotumika vibaya hivi kwamba nyingi ya viungo hivyo kwenye huduma zetu vinakiuka sehemu za taka au usalama mtandaoni za Viwango vya Jumuiya.