Uchi, Dhuluma na Unyanyasaji wa Watoto Kingono

Maelezo ya sera

BADILISHA KUMBUKUMBU
Utaratibu wa Sera
Haturuhusu maudhui au shughuli zinazowanyanyasa kingono au kuwahatarisha watoto. Tunapogundua unyanyasaji wa mzazi dhidi ya mtoto, tunaripoti katika Kituo cha Taifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC), kwa kuzingatia sheria inayotekelezwa. Tunafahamu kuwa wakati mwingine watu wanashiriki picha za uchi za watoto wao binafsi kwa nia nzuri; hata hivyo, kwa kawaida tunaziondoa picha hizi kwa sababu ya uwezekano wa matumizi mabaya na wengine na kusaidia kuepuka uwezekano wa watu wengine kutumia upya au kutumia vibaya picha.
Pia tunashirikiana na wataalamu wa nje, ikijumuisha Bodi ya Ushauri ya Usalama wa Meta, ili kujadili na kuboresha sera zetu na utekelezaji katika masuala ya usalama wa mtandaoni, hususan kulingana na watoto. Jifunze zaidi kuhusu teknolojia tunayotumia kupambana dhidi ya matumizi mabaya ya mtoto.
Usichapishe:
Unyanyasaji wa watoto kingono
Maudhui, shughuli, au mwingiliano unaotishia, kuonyesha, kusifu, kusaidia, kutoa mafunzo, inayotoa taarifa ya lengo, inayokubali kuhusika katika au kushiriki viungo vya unyanyasaji wa watoto kingono (ikijumuisha watoto wa kweli, watoto wachanga, au wadogo au maonyesho yasiyo ya halisi yenye mfano wa mwanadamu, kama vile katika sanaa, maudhui yanayozalishwa na AI, wahusika wa kubuni, wanasesere, n.k). Hii inajumuisha, lakini si tu kwa:
  • Kujamiana
    • Kitendo dhahiri cha kujamiiana au ngono ya kinywa, inafafanuliwa kama mdomo au sehemu nyeti zikiingia au zikishikana na sehemu nyeti za mtu mwingine au mkundu, wakati angalau sehemu ya siri ya mtu au mkundu unaonekana.
    • Kujamiana kunakodokezwa au ngono ya kinywa, ikiwemo wakati mgusano uko karibu kufanyika au hauonekani moja kwa moja.
    • Usisimuaji wa sehemu za siri au mkundu, ikiwemo wakati shughuli iko karibu kufanyika au haionekani moja kwa moja kwa moja.
    • Yoyote hapo juu inayojumuisha mnyama.
  • Watoto walio na vipengele vya ngono, ikijumuisha lakini si tu:
    • Vikwazo
    • Ishara za kuchangamsha
    • Kulenga sehemu za siri au mkundu
    • Kuwepo kwa mtu mzima aliye na msisimko wa kushiriki ngono
    • Kuwepo kwa vifaa vya ngono au matumizi ya kitu chochote kwa ajili ya kusisimua ngono, kujitosheleza au unyanyasaji wa kingono
    • Mavazi ya ngono
    • Kuvua nguo
    • Mazingira yaliyoandaliwa (kwa mfano, kwenye kitanda) au kupigwa kwa njia ya kitaalamu (ubora/mlengo/pembe)
    • Kupusiana mdomoni
    • Kusisimua chuchu za binadamu au kufinya matiti ya mwanamke (ISIPOKUWA katika muktadha wa kunyonyesha)
    • Uwepo wa bidhaa za shughuli ya ngono
  • Maudhui yanayohusisha watoto wakiwa katika muktadha wa makago ya kingono
  • Maudhui ambayo yanasaidia, kuunga mkono, kutetea au kuhimiza kushiriki katika kuwanajisi watoto isipokuwa inajadiliwa kwa upande wote katika muktadha wa kiafya.
  • Maudhui ambayo yanatambua au kudhihaki waathirika watoto wanaotumiwa vibaya kingono kwa jina au picha
Uombaji ngono
Maudhui yanayoshawishi maudhui ya ngono au shughuli zinazoonyesha au kuhusisha watoto, yanafafanuliwa kama:
  • Nyenzo za Dhuluma ya Kingono kwa Watoto (CSAM)
  • Taswira za uchi za watoto wa kweli au wasio wa kweli
  • Taswira za ngono za watoto wa kweli au wasio wa kweli
Mitangamano isiofaa na watoto
Maudhui yanayojumuisha au kuwezesha miingiliano isiyofaa kwa watoto, kama vile:
  • Kuomba, kuratibu au kupanga kufanya ngono na watoto
  • Kuwashawishi watoto kushiriki ngono kupitia mazungumzo ya ngono au kutoa, kuonyesha, kupata au kuomba nyenzo za ngono kwa watoto au kutoka kwa watoto, kupitia kufichuliwa kwa makusudi au kwa ujumbe wa faragha.
  • Kujihusisha na mazungumzo ya kudokeza ngono katika ujumbe binafsi na watoto
  • Kupata au kuomba nyenzo za kingono kutoka kwa watoto katika ujumbe binafsi
Taswira za mahaba na utozaji pesa kwa nguvu kwa sababu za kingono
Maudhui ambayo yanajaribu kuwatumia watoto halisi kwa:
  • Kulazimisha watu kukupa pesa, mapendeleo au taswira za mahaba kwa kutishia kufichua taswira za kweli au zisizo za kweli za mahaba au maelezo nyeti
  • Kushiriki, kutishia, au kusema kwa nia ya kushiriki mazungumzo ya ngono ya kibinafsi au taswira za mahaba za kweli au zisizo za kweli
Kuwasawiri watoto kingono
  • Maudhui (yakijumuisha picha, video, sanaa ya ulimwengu halisi, kidijitali na maelezo ya maneno) yanayoonyesha watoto wa kweli au wasio wa kweli kwenye muktadha wa kingono
  • Makundi, Kurasa ,na Wasifu zinazolenga kuwafanyisha watoto wa kweli au wa kubuni kwa muktadha wa kingono
Uchi wa mtoto
Maudhui yanayoonyesha picha za uchi za mtoto wa kweli au asiye wa kweli ambapo uchi unafafanuliwa kama:
  • Picha za karibu za viungo vya siri vya watoto wa kweli au wasio wa kweli
  • Picha za kweli au zisizo za kweli za watoto wachanga, zinazoonyesha:
    • Sehemu za siri zinazoonekana hata iwapo zimefunikwa au kufungwa kwa mavazi ya uwazi
    • Mkundu unaoonekana na/au mwonekano kamili wa makalio yakiwa uchi
  • Picha za kweli au zisizo za kweli za watoto, zinazoonyesha:
    • Sehemu za siri zinazoonekana (ikiwemo sehemu za siri zilizofunikwa kwa mavuzi au mavazi ya uwazi)
    • Mkundu unaoonekana na/au mwonekano kamili wa makalio yakiwa uchi
    • Chuchu za kike zisizofunikwa
    • Hakuna mavazi kuanzia shingoni hadi kwenye goti - haya kama sehemu za siri au chuchu za kike hazionekani
  • Isipokuwa taswira isiyo ya kweli ni ya madhumuni ya afya au ni taswira isiyo ya ngono ya uchi wa mtoto katika sanaa ya ulimwengu halisi.
Matumizi mabaya ya watoto yasiyokuwa ya kingono
Video au picha ambazo zinaonyesha dhuluma isiyo ya ngono ya mtoto wa kweli au asiye wa kweli bila kujali dhamira ya kushiriki, isipokuwa taswira hizo zinatokana na sanaa ya ulimwengu halisi, katuni, filamu au michezo ya video.
Maudhui yanayosifu, kusaidia, kuunga mkono, kutetea, kutoa maelekezo ya au kuhimiza kushiriki katika matumizi mabaya ya watoto yasiyo ya kingono
Mbali na kuondoa akaunti zinazokiuka sera zetu za Unyanyasaji wa Kingono, Matumizi mabaya na Uchi kwa Watoto (CSEAN), wakaguzi wetu na mifumo otomatiki huzingatia wigo mpana wa ishara ili kusaidia kuzuia mwingiliano unaoweza kuwa usiotakikana au usio salama.
  • Tunaweza kulemaza akaunti au kuzuia ufikiaji wa bidhaa na vipengele (kwa mfano, uwezo wa kufuata akaunti fulani) kwa watu wazima kulingana na mwingiliano wao na akaunti nyingine, utafutaji au mwingiliano na maudhui yanayokiuka (k.m. kupenda au kuhifadhi), au uanachama katika jumuiya (km Vikundi) ambavyo tumeondoa kwa kukiuka sera zetu.
Kwa maudhui yafuatayo, tunajumuisha skrini ya onyo ili watu wafahamu kuwa maudhui yanaweza kuvuruga akili na kupunguza uwezo wa kutazama maudhui kwa watu wazima, wa umri wa miaka kumi na nane na zaidi:
  • Video au picha zinazoonyesha maafisa wa polisi au wanajeshi wakifanya dhuluma isiyo ya ngono ya mtoto
  • Video au picha za dhuluma isiyo ya ngono ya mtoto, wakati watekelezaji wa sheria, mashirika ya ulinzi wa watoto, au washirika wa usalama wa kuaminika wanaomba tusiondoe maudhui kwenye jukwaa kwa kusudi dhahiri la kumrudisha mtoto salama
Kwa maudhui yafuatayo, tunajumuisha ilani kwenye skrini ili watu wajue kwamba maudhui yanaweza kuwa ya kutatanisha kwa baadhi ya watu:
  • Video au picha za mtoto kulazimishwa kwa nguvu ndani ya maji katika muktadha wa mila ya kidini
Kwa Viwango vya Jumuiya vifuatavyo, tunahitaji maelezo ya ziada na/au muktadha ili kutekeleza:
Kwa maudhui yafuatayo, tunajumuisha lebo ya onyo ili watu wafahamu kuwa maudhui yanaweza kuwa nyeti:
  • Picha iliyochapishwa na shirika la habari ambayo linaonyesha uchi wa watoto katika muktadha wa njaa, uangamizaji wa kabila, uhalifu wa kivita, au uhalifu dhidi ya ubinadamu, isipokuwa imeambatana na maelezo mafupi ya ukiukaji au kushirikiwa katika muktadha wa ukiukaji, katika hali hiyo maudhui huondolewa
Tunaweza kuondoa taswira inayoonyesha matokeo ya dhuluma isiyo ya ngono ya mtoto inaporipotiwa na washirika wa vyombo vya habari, NGO au washirika wengine wa usalama wanaoaminika.
Tunaweza kuondoa maudhui ambayo yanawatambulisha wahasiriwa wa unyanyasaji wa kingono wa watoto kupitia njia nyingine isipokuwa jina au taswira ikiwa maudhui yanajumuisha maelezo ambayo huenda yakasababisha mtu huyo kutambuliwa.
Tunaweza kuondoa maudhui yaliyoundwa kwa madhumuni ya kutambua mtoto wa kibinafsi ikiwa kuna hatari ya usalama wa mtoto huyo, inapoombwa na Watekelezaji wa Sheria, Serikali, Mshirika Anayeaminika, au maudhui hayo yameripotiwa na mtoto huyo au mzazi/mlezi wa kisheria wa mtoto
Hali ya matumizi ya mtumiaji
Tazama mifano kadhaa ya jinsi utekelezaji unavyoonekana kwa watu kwenye Facebook, kama vile: inavyoonekana kuripoti kitu ambacho unafikiri hakipaswi kuwa kwenye Facebook, kuambiwa kuwa umekiuka Viwango vyetu vya Jumuiya na kuona skrini ya onyo juu ya maudhui fulani.
Dokezo: Tunaendelea kuboresha, kwa hivyo kile unachokiona hapa kinaweza kupitwa na wakati kiasi ikilinganishwa na kile tunachotumia sasa.
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Kuripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Mawasiliano ya baada ya ripoti
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Hali ya kuondoa
HALI YA MATUMIZI YA MTUMIAJI
Skrini za onyo
Data
Tazama Ripoti ya sasa ya Utekelezwaji wa Viwango vya Jumuiya
Utekelezaji
Tuna sera sawa ulimwenguni kote, kwa ajili ya kila mtu kwenye Facebook.
Timu za ukaguzi
Timu yetu ya kimataifa ya wakaguzi zaidi ya 15,000 hufanya kazi kila siku kuweka watu kwenye Facebook kuwa salama.
Ushiriki wa mshikadau
Wataalamu wa nje, wasomi, mashirika yasiyo ya faida na watungaji sera husaidia kuweka Viwango vya Jumuiya ya Facebook.
Pata usaidizi wa unyanyasaji wa kingono wa watoto, dhuluma na uchi
Jifunze unachoweza kufanya ukiona kitu kwenye Facebook ambacho kinakiuka Viwango vyetu vya Jumuiya.
Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi