Viwango vya Jumuiya

Viwango vya Jumuiya ya Facebook vinabainisha kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa kwenye Facebook, Instagram, Messenger na Threads.
Utangulizi
Viwango hivi vinategemea maoni kutoka kwa watu na ushauri wa wataalamu katika nyanja kama vile teknolojia, usalama wa umma na haki za binadamu. Ili kuhakikisha sauti ya kila mtu inathaminiwa, tunachukua tahadhari kubwa kuunda viwango vinavyojumuisha maoni na imani tofauti, haswa kutoka kwa watu na jumuiya ambazo zinaweza kupuuzwa au kutengwa.
Kila siku, watu hutumia Facebook, Instagram, Messenger na Threads kushiriki hali zao, kuwasiliana na marafiki na familia na kujenga jumuiya. Huduma zetu huwezesha mabilioni ya watu kujieleza kwa uhuru katika nchi na tamaduni na mbalimbali kwa lugha nyingi.
Meta inatambua jinsi ilivyo muhimu kwa Facebook, Instagram, Messenger na Threads kuwa maeneo ya watu kujihisi wamewezeshwa kuwasiliana, na tunawajibikia kikamilifu jukumu letu la kupiga marufuku matumizi mabaya ya huduma. Ndio sababu tuliunda viwango vya kile kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa kwenye huduma hizi.
Tafadhali kumbuka kuwa toleo la Kiingereza cha Marekani cha Viwango vya Jumuiya linaakisi seti ya sera zilizosasishwa hivi karibuni zaidi na linafaa kutumiwa kama waraka msingi.
Kusisitiza Kujitolea Kwetu kwa Sauti
Lengo la Viwango vyetu vya Jumuiya ni kuunda mahali pa kujieleza na kuwapa watu sauti. Meta inataka watu wawe na uwezo wa kuzungumza kwa uwazi kuhusu masuala ya umuhimu kwao, iwe kupitia maoni yaliyoandikwa, picha, muziki, au vyombo vingine vya sanaa, hata ikiwa baadhi ya watu wanaweza kukataa au kuyapata kuweza kukataliwa. Katika baadhi ya mifano, tunaruhusu maudhui—ambayo vinginevyo yanakiuka viwango vyetu—iwapo yanastahili kuwa habari na yanakidhi matakwa ya umma. Tunafanya hivi tu baada ya kupima thamani ya matakwa ya umma dhidi ya hatari za madhara, na kuangalia viwango vya kimataifa vya haki za kibinadamu kufanya maamuzi haya. Katika hali nyingine, tunaweza kuondoa maudhui ambayo yanatumia lugha isiyoeleweka au iliyodokezwa wakati muktadha wa ziada unaturuhusu kuelewa kuwa maudhui hayo yanakiuka viwango vyetu.
Kujitolea kwetu kuruhusu watu kujieleza ni muhimu, lakini tunatambua kwamba mtandao hutoa nafasi mpya na nyingi za matumizi mabaya. Kutokana na sababu hizi, tunapoweka kikomo cha kujieleza, tunaifanya katika kuhudumia moja au zaidi ya thamani zifuatazo:
UHALALI
Tunataka kuhakikisha kuwa maudhui ambayo watu wanaona ni ya kweli. Tunaamini kuwa uhalisi huunda mazingira bora ya kushiriki, na hiyo ndiyo sababu hatutaki watu wanaotumia huduma zetu kuwakilisha vibaya utambulisho wao au kile wanachokifanya.
USALAMA
Tumejitolea kufanya Facebook, Instagram, Messenger na Threads kuwa mahali salama. Tunaondoa maudhui ambayo yanaweza kuchangia hatari ya madhara kwa usalama wa kimwili wa watu. Maudhui ambayo hutishia watu yana uwezo wa kudhoofisha, kutenga au kunyamazisha wengine na hakukubaliki kwenye huduma zetu.
FARAGHA
Tumejitolea kulinda faragha na maelezo ya kibinafsi. Faragha huwapa watu uhuru wa kujiamini, kuchagua jinsi na wakati wa kushiriki kwenye huduma zetu na kuunganisha kwa urahisi zaidi.
HADHI
Tunaamini kwamba watu wote wako sawa kihadhi na haki. Tunatarajia kwamba watu wataheshimu hadhi ya wenzao na hawatadhulumu au kushusha hadhi wenzao.
Viwango vya Jumuiya
Viwango vyetu vya Jumuiya vinatumika kwa kila mtu, kote ulimwenguni na kwa aina zote za maudhui, ikiwa ni pamoja na maudhui yanayozalishwa na AI.
Kila sehemu ya Viwango vyetu vya Jumuiya inaanza kwa “Utaratibu wa Sera” unaobainisha malengo ya sera hii na kufuatwa na mikondo mahususi ya sera inayobainisha:
Maudhui ambayo hayaruhusiwi; na
Maudhui ambayo yanahitaji maelezo au muktadha wa ziada ili kutekeleza, maudhui ambayo yanaruhusiwa lakini yanawekewa skrini ya onyo au maudhui ambayo yanaruhusiwa lakini yanatazamwa na watu wazima wenye umri wa miaka 18 au zaidi.